Simba yaja na Back to school - EDUSPORTSTZ

Latest

Simba yaja na Back to school

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Klabu ya Simba leo imetangaza kuzindua program ya Back to School ambayo ni mahsusi kupelekwa mashuleni kwa ajili ya kuongeza mashabiki wapya wa Simba


Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Mtendaji Mkuu wa Simba Imani Kajula amesema Simba itapita mashuleni kwa ajili ya kutafuta mashabiki wapya pamoja na kusaka vipaji vipya vya wachezaji ambao watawaendeleza


Mkuu wa Programu za vijana, Patrick Rweyemamu amepewa jukumu la kusimamia mchakato huo katika mashule


Katika sehemu ya mpango huo, Kajula amesema kwenye mechi zake Simba itatoa mialiko kwa shule mbalimbali ili kuwapa fursa watoto kujifunza na kwendana na utamaduni wa Simba tangu utotoni


Mpango huo utafanyika sambamba kwa ushirikiano na Washirika wa Simba benki za CRDB na NMB. Benki hizo zimeandaa kadi maalum zinazojulikana kama Simba Caps (Mtoto wa Simba)


"Tumezindua Programu maalum tuliyoipa jina la Back to School kwa ajili ya kutembelea shule mbalimbali nchi nzima ili kuandaa mashabiki wapya pamoja na kuvumbua vipaji kwakuwa makocha wetu watakuwa wanatembelea huko," alisema Kajula



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz