Yanga kuelekea Rwanda September 14 - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga kuelekea Rwanda September 14

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Msafara wa kikosi cha Yanga ukijumuisha mashabiki utaondoka nchini Septemba 14 kuelekea Rwanda kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya El Merrikh ambao utapigwa Septemba 16


Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari mapema leo, Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema timu itaondoka kwa usafiri wa ndege, kutakuwa na usafiri maalum wa mabasi kwa ajili ya mashabiki


Kamwe ametangaza gharama ya safari ya kwenda na kurudi Rwanda ni Tsh 150,000/- ambapo kwa shabiki atakayehitaji kusafiri lazima awe na hati ya kusafiria


"Msafara wetu utaondoka nchini Septemba 14, tuta safiri na mashabiki wengi na naamini tunaenda kuweka rekodi ya kujaza uwanja wa Pele, Rwanda"


"Mashabiki ni wengi wanaitaka hii safari, pia tuna mashabiki wa Yanga wapo Kigali.Tarehe 14 msafara wa mashabiki utaanza safari kutoka Dar - Kigali saa 11 alfajiri na tutalala Kahama"


"Gharama ya safari ni TSH 150,000/- na mashabiki anapaswa kuwa na hati ya kusafiria au kibali cha safari," alisema Kamwe


Akizungumzia maandalizi ya kikosi, Kamwe amesema timu imerejea mazoezini baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki


Siku ya Jumapili Yanga itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ambayo itatangazwa baadae. Hata hivyo amesema Yanga inatoa mwaliko kwa timu yoyote ambayo inataka kujipima na Yanga katika uwanja wowote


"Tunatarajia kuwa na mchezo wa kirafiki siku ya jumapili. Tutatangaza tunacheza na timu gani. Hata hivyo tunatoa fursa kwa timu yoyote inaweza kuomba mchezo wa kirafiki na sisi tutacheza popote pale"Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz