Novatus azipiga dakika zote 90 Ligi ya Mabingwa - EDUSPORTSTZ

Latest

Novatus azipiga dakika zote 90 Ligi ya Mabingwa

 Novatus Dismas Miroshi

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Kiungo wa Kimataifa wa Tanzania, Novatus Dismas Miroshi usiku wa jana amecheza kwa dakika zote 90 timu yake, FC Shakhtar Donetsk y Ukraine ikichapwa mabao 3-1 na FC Porto ya Ureno katika mchezo wa kwanza wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Volksparkstadion Jijini Hamburg, Ujerumani.


Mabao ya FC Porto yamefungwa na washambuliaji wake Mbrazil, Wenderson Galeno mawili dakika ya nane na 15 na Muiran Mehdi Taremi dakika ya 29.


Bao pekee la FC Shakhtar Donetsk inayolazimika kuchezea mechi zake za nyumbani Ujerumani kutokana na machafuko yanayoendelea nchini kwao kufuatia uvamizi wa majeshi ya Urusi limefungwa na mshambuliaji wake Mvenezueala, Kevin Kelsy dakika ya 13.


Miroshi anakuwa Mtanzania wa tatu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya Athumani Machuppa na Mbwana Samatta na mchezaji wa tatu kwa ujumla kutoka nchi hii kucheza michuano ya Ulaya baada ya Kassim Manara kucheza iliyokuwa michuano ya Kombe la Washindi.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz