Kocha Singida afunguka sababu ya kubwaga manyanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Kocha Singida afunguka sababu ya kubwaga manyanga

 Kocha Singida afunguka sababu ya kubwaga manyanga

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Kocha wa Singida BS, Ernst Middendorp amesema sababu kubwa iliyomfanya aachane na klabu hiyo ni kitendo cha kuingiliwa katika majukumu yake.


Akizungumza kupitia mahojiano yaliyorushwa Wasafi FM, kocha huyo alisema ilifika wakati aliona huko mbeleni atakuja kupangiwa hadi wachezaji jambo ambalo hataweza kulivumilia.


"Mimi ni binadamu na ni udhaifu wangu katika kuamua mambo nina jazba, mazingira ya Singida yamenishinda sababu nimeona wananiingilia. Nilizungumza na Waziri wa Fedha na viongozi wengine nikawaambia kwa kweli sitaweza," alisema kocha huyo.


Kocha huyo alisema, mara baada ya kucheza na Future na kupata ushindi wa goli 1-0, kiliitishwa kikao ambacho hakikuwa na ajenda na ndipo walipoanza kumhoji kwa nini hajawatumia wachezaji fulani katika kikosi cha kwanza.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz