Simba vs Coastal Union warudishwa uwanja Uhuru tena - EDUSPORTSTZ

Latest

Simba vs Coastal Union warudishwa uwanja Uhuru tena

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya Simba dhidi ya Coastal Union ambao utapigwa kesho Alhamisi Septemba 21, utachezwa katika uwanja wa Uhuru kama ratiba ilivyopangwa awali


Kulikuwa na taarifa ya mchezo huo kupelekwa uwanja wa Azam Complex, lakini kulingana na ratiba iliyotolewa na Bodi ya Ligi, mchezo huo umebaki dimba la Uhuru ambalo Simba walichagua kulitumia wakati uwanja wa Benjamin Mkapa ukiendelea na ukarabati


Kikosi cha Simba kilirejea juzi kutoka Zambia baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Power Dynamos uliomalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2


Wekundu hao wa Msimbazi waliingia moja kwa moja kambini na leo watakamilisha maandalizi yao tayari kuwakabili Coastal Union ambao tayari wako jijini Dar es salaam


Simba itatumia mchezo huu kama sehemu ya maandalizi yake kuelekea mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Power Dynamos ambao utapigwa wiki ijayo kwenye uwanja wa Azam ComplexDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz