Kuziona Yanga vs Al Merrikh buku 10 tu - EDUSPORTSTZ

Latest

Kuziona Yanga vs Al Merrikh buku 10 tu

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema mandalizi kuelekea mchezo wa mkondo wa pili kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merrikh, yanaendelea vizuri


Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Kamwe amesema baada ya miaka mingi kutocheza hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa, hii ni nafasi kubwa kwa Yanga kufanikisha lengo 


Kamwe amesema wamezisikia kauli za kocha wa Al Merrikh kuwa Yanga inaogopeka barani Afrika, lakini wanamwambia maneno yake hayawezi kuwafanya wakabweteka ukubwa au udogo watauonyesha katika mchezo huo


"Maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya AL Merrikh yanaendelea vizuri, jana tulikuwa na session moja na leo tuna session mbili, asubuhi wachezaji wamefanya mazoezi na pia watafanya jioni"


"Tumezisikia kauli za kocha Al Merrikh anasema Yanga inaogopwa barani Afrika lakini sisi tunamwambia asitutoe kwenye reli, tunamsubiri aje uwanja wa Azam Complex tupambane nae katika mchezo ambao tunajua utakuwa sio rahisi," alisema Kamwe


Kamwe ametangaza viingilio vya mchezo huo VIP A ni Tsh 50,000/-, VIP B ni Tsh 20,000/- na Mzunguuko ni Tsh 10,000/-


Pia kutakuwa na tiketi za Royal zinazopatikana kwa Tsh 100,000/-


Tiketi tayari zinapatikana kupitia mitandao ya simu na vituo vingine ambavyo vitatangazwa


Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kununua tiketi mapema kwa kufahamu ukubwa wa uwanja wa Azam Complx unachukua watu wachacheDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz