Kocha Al Merrikh: Yanga inaogopeka Afrika - EDUSPORTSTZ

Latest

Kocha Al Merrikh: Yanga inaogopeka Afrika

 Kocha Al Merrikh: Yanga inaogopeka Afrika

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Kocha huyo anayokumbukumbu ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 wakiwa nyumbani katika mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Al Merrikh wanatarajiwa kurudiana na Yanga katika mchezo wa mzunguko wa pili wakiwa ugenini katika Uwanja wa Azam Comlex mchezo huo unatarajiwa kufanyika Septemba 30.


Akizungumza kuelekea katika mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga kocha huyo alisema kuwa: “Ukisema kuwa tunahofia kukutana na Yanga hapana, hilo halina ukweli kwa kuwa tayari tulishacheza nao na tulipoteza mchezo wa kwanza, ukweli ni huu kuwa Yanga kwa sasa ni tishio Afrika kulingana na walivyo.


“Ni timu ambayo inacheza vyema na inapata matokeo hivyo ni lazima tuwaheshimu kulingana na ubora wao huo, tunakwenda kurudiana na timu ambayo ni ngumu lakini wakiwa na faida kubwa ya wao kucheza kwao.


“Ambacho kipo kwa upande wetu ni kuendelea kujipanga kwa ajili ya kuhakikisha kuwa tunafanya vyema, kuwa na mipango mizuri ya kupata matokeo tukiwa ugenini, nia na malengo yetu ni kwenda hatua inayofuata na tuna matumaini hayo na wala hatujakata tama,” alisema kocha huyo.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz