Kocha Azam FC asimamishwa - EDUSPORTSTZ

Latest

Kocha Azam FC asimamishwa

 Kocha wa Azam FC, Youssouf Dabo

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemzuia rasmi Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssouph Dabo, raia wa Senegal kusimama kwenye benchi la ufundi la timu hiyo kutokana na sababu za kutokidhi vigezo ambavyo vinatakiwa.


Dabo ambaye tangu ametua nchini amekuwa akikiongoza kikosi hicho amezuiwa kutokana na Leseni A ya UEFA aliyonayo kutokidhi vigezo vya kanuni za soka la Tanzania ambazo haziruhusu kuwa kocha mkuu wa Ligi Kuu.


Chanzo cha kuaminika kutoka TFF kimesema kuwa, Dabo hatambuliki kama kocha mkuu hivyo kutokana na leseni aliyonayo anaruhusiwa kusimama benchi akiwa msaidizi na viongozi wa Azam tayari wanalijua hilo.


“Mwanzo alikuwa anakaa na kutambulika kama kocha mkuu kwa sababu awali walisema atakwenda kuongeza elimu yake, lakini baada ya kuona kimya na maneno mengi tukaona tufuate kanuni tulizojiwekea,” kilisema chanzo.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz