Diarra, Aziz Ki kuiwahi Al Merrikh - EDUSPORTSTZ

Latest

Diarra, Aziz Ki kuiwahi Al Merrikh

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mlinda lango Djigui Diarra na kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki huenda wakaungana na kikosi cha Yanga nchini Rwanda tayari kwa mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Merrikh ya Sudan

Mchezo huo utapigwa siku ya Jumamosi, Septemba 16 katika uwanja wa Pele, Kigali majira ya saa 10 jioni (saa 9 Rwanda)


Aziz Ki alikuwa Morocco na timu ya Taifa ya Burkina Faso ambapo jana walicheza mechi ya Kimataifa ya kirafiki dhidi ya wenyeji wao Morocco wakikubali kipigo cha bao 1-0

Mechi hiyo awali iliahirishwa baada ya kutokea tetemeko kubwa la ardhi lililosababisha maafa makubwa nchini Morocco


Diarra jana alikuwa langoni kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Ivory Coast ambao ulimalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana

Huo ulikuwa mchezo wa tatu mfululizo Diarra anakaa langoni na kudaka kwa dakika zote 90

Ili kuepuka uchovu wa kuunganisha safari, wachezaji hao huenda wakasafiri moja kwa moja Rwanda na wataungana na wenzao ambao wataondoka nchini kesho Alhamisi, saa 11 jioniDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz