Yanga watangaza siku ya kurudi Skudu Makudubela - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga watangaza siku ya kurudi Skudu Makudubela

 Winga wa Yanga, Skudu Makudubela

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga, Alli Kamwe akizungumza leo na waandisi wa habari amesema kesho siku ya Ijumaa Mahlatse Makudubela 'Skudu' atarejea nchini akitokea nchini kwao Afrika Kusini alipokwenda kushughulikia hati yake ya kusafiria (passport) ambayo imejaa.


"Skudu kweli alisafiri kwenda Afrika Kusini na kesho Ijumaa atarejea nchini Kocha Gamondi akitaka kumtumia Jumamosi ni maamuzi yake , amepona kabisa na tuliwaaambia amekwenda kushugulikia passport yake ya kusafiria"


Skudu alishindwa kuendelea na mchezo katika Nusu fainali Ngao ya Jamii dhidi ya Azam, baada ya kuchezewa rafu dakika ya saba na kiungo wa Azam, James Akaminko.


Na Yanga iliichapa Azam 2-0 mabao yalifungwa na Aziz KI na Clement Mzize ambayo yamefungwa katika dakika 10 za mwisho za mchezo huo.


Skudu ameweka rekodi ndani ya Yanga ya kuwa mchezaji wa kwanza raia wa Afrika Kusini kuwatumikia mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya NBC na Kombe la Shirikisho la Azam.


Mbali na Marumo staa huyo pia amewahi kuzichezea timu za Afrika Kusini, Chippa United na Orlando Pirates kwa mafanikio makubwa, anatajwa kuwa mmoja kati ya wachezaji wenye uzoefu sana kwenye Ligi Kuu Afrika Kusini.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz