Tetesi za Usajili Barani ulaya Leo Jumatano - EDUSPORTSTZ

Latest

Tetesi za Usajili Barani ulaya Leo Jumatano

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mchezaji huru Alexis Sanchez anapangwa kurejea Inter Milan kama klabu itakubaliana na maombi yake.


Chelsea wanashikilia dau la £8m kwa vilabu ambavyo vinamuhitaji winga Callum Hudson-Odoi, ambaye sasa anapokea alipokea kutoka kwa Nottingham Forest na Everton pamoja na Fulham.


Ujio unaokaribia wa jeremy Doku katika klabu ya Manchester City unaweza kufanya uwezekano mkubwa zaidi kwamba Cole Palmer atawaacha mabingwa wa Ligi ya Premier msimu huu wa joto.


Huku vilabu vingi vya Ligi ya Premier wakisubiri kutoa ofa kwa nyota huyo wa U21 wa Uingereza.

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Nottingham Forest imemgeukia kiungo wa Chelsea, Andrey Santos wakati wakijaribu kuimarisha safu yao ya kiungo, jambo ambalo linaweza kumpa Mauricio Pochettino kuongeza kasi katika kumsaka mshambuliaji wao Brennan Johnson.


Liverpool na Bayern Munich wamefanya mazungumzo zaidi kuhusu dili la kiungo Ryan Gravenberch ambaye sasa anaonekana kupatikana zaidi na klabu hiyo ya Bundesliga.


Manchester United na Bayern Munich zote zimeonyesha nia ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Paris Saint-Germain Marco Verratti, ambaye yuko huru kuondoka katika klabu hiyo ya Ligue 1 msimu huu wa joto.


Klabu ya West Ham United iko tayari kutangaza kumsajili mlinzi wa Ugiriki Konstantinos Mavropanos baada ya madai kuwa ameshinda vipimo vyake.


Maelezo madogo ya kimkataba yamechelewesha tangazo hilo.


Chelsea ilishindwa kufuata itifaki zinazohitajika katika majaribio yao ya kumrejesha Michael Olise Stamford Bridge na mchezaji huyo hatimaye kusaini mkataba mpya huko Crystal Palace.


Manchester City wamekubali makubaliano ya kibinafsi na Jeremy Doku juu ya mkataba wa muda mrefu ambao ulikuwa na kifungu chenye thamani ya euro 60m (£51.3m) kilichokubaliwa na Rennes kwa winga huyo wa Ubelgiji, 21.

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

West Ham walikuwa wamekubali mkataba wa £85m ya kimsingi na Manchester City ili kuweza kumuuza Lucas Paqueta.


Makubaliano hayo yamevunjika kutokana na kiungo huyo wa kati wa Brazil, 25, kuchunguzwa kwa ukiukaji wa kanuni za kamari.


Bayern Munich na Liverpool zote zimeonyesha nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 27, kutoka Manchester City.


Brighton wanakaribia kukamilisha usajili wa pauni milioni 25 na kiungo wa kati wa Lille raia wa Cameroon Carlos Baleba, 19.


West Ham wamewasilisha ombi rasmi la takriban £35m kumnunua mshambuliaji wa Bournemouth na Uingereza Dominic Solanke mwenye umri wa miaka 25.


Paris St-Germain (PSG) bado wana matumaini wanaweza kumshawishi Kylian Mbappé kuongeza mkataba mpya baada ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa, 24, kukutana na maafisa wa kundi la umiliki wa klabu hiyo ya Qatar.


Licha ya mchezaji huyo kuhusishwa na kuhamia Real Madrid mkataba wake utakapokamilika, majira ya joto.


West Ham wanafanya mazungumzo na Sevilla kuhusu kumsajili mshambuliaji wao wa Morocco Youssef En-Nesyri, 26.


Chelsea wamekubali mkataba wa pauni milioni 14 kwa mlinda mlango wa New England Revolution wa Serbia Djordje Petrovic, 23.


Fulham wanakabiliwa na ushindani mpya kwa Callum Hudson-Odoi wa Chelsea baada ya Everton na Nottingham Forest kuingia katika kinyang'anyiro cha kumsajili winga huyo, 22.


Chelsea inasalia kwenye mazungumzo kuhusu uhamisho wa Folarin Balogun wa Arsenal.


Mshambuliaji huyo wa Marekani, 22, tayari ameshakubaliana na The Blues.


Fulham wako tayari kukabiliana na Tottenham kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Gift Orban, 21, kutoka Gent ya Ubelgiji.


Lazio wameanzisha tena mazungumzo na Tottenham kuhusu mpango wa kumnunua mlinda mlango wa Ufaransa Hugo Lloris mwenye umri wa miaka 36.


Aston Villa wameonyesha nia ya kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Ureno Nuno Tavares, 23, kutoka Arsenal.


Mshambulizi wa Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 18, yuko kwenye rada za Arsenal kwa dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.


Brentford wamefanya uchunguzi kuhusu uwezekano wa kumnunua winga wa Leeds United na Colombia Luis Sinisterra, 24.


Manchester City wanakaribia kukubaliana kandarasi mpya na winga wa Ureno Bernardo Silva, 29, na beki wa kulia wa Ureno Bernardo Silva, 29, na beki wa kulia wa Uingereza Kyle Walker, 33.


Liverpool FC wanasubiri matokeo ya majadiliano kati ya kiungo wa Bayern Munich Ryan Gravenberch, 21, na mkufunzi Thomas Tuchel kuhusu mustakabali wa Mholanzi huyo.


Liverpool wapo tayari kukubaliana na masharti yoyote kwa sababu wanampango na mchezaji huyo.


Manchester United wanataka kusajili kiungo na mlinda mlango kabla ya tarehe ya mwisho wa usajili, lakini wanahitaji kupunguza kikosi chao kwanza.

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Mshambulizi wa Uingereza Mason Greenwood, 21, anatarajiwa kutafuta ofa nchini Uturuki au Italia baada ya pande zote kukubaliana kuondoka Manchester United msimu huu.


Kufuatia uchunguzi wa ndani wa klabu hiyo Inasemekana kuwa Manchester United hawana mpango naye mara baada ya kutoka katika kifungu cha kukaa nje karbu mwaka mmoja kwa tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia na kosa la ubakaji.


Kocha wa uingereza wa wanawake Sarina Wiegman atakuwa kwenye fremu ya kuwa kocha wa timu ya taifa ya wanaume ya Uholanzi wadhifa huo utakapopatikana hivi karbuni.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz