Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Helmey alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la Yanga lililoshinda mataji sita katika misimu miwili mfululizo likiongozwa na Nasreddine Nabi
Aliondoka Yanga baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu uliopita. Awali alikuwa kwenye mpango wa kutua Kaizer Chiefs na Nabi
Hata hivyo mpango huo haukufanikiwa, Nabi amejiunga na FAR Rabat, mabingwa wa Ligi Kuu ya Morocco na Helmey sasa ametua Orlando ambao ni wapinzani wa Kaizer Chiefs
Mafanikio ya Yanga katika michuano ya Kimataifa msimu uliopita yamewapa ulaji waliokuwa makocha katika benchi la ufundi
Aliyekuwa Kocha Msaidizi Cedric Kaze yeye ni kocha mkuu wa Namungo Fc wakati aliyekuwa Kocha wa magolikipa Milton Nienov amerejea kwao Brazil sasa akiwa kocha mkuu wa moja ya klabu inayoshiriki Serie B nchini humo
No comments:
Post a Comment