Tunayataka Makombe yote:- Robertinho - EDUSPORTSTZ

Latest

Tunayataka Makombe yote:- Robertinho

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amesema kikosi chake kimeimarika na sasa malengo yao ni kuona wanashinda mataji


Simba imerejea Tanzania Alfajiri ya leo wakitokea Uturuki ambako waliweka kambi ya wiki tatu kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya


Robertinho amewapongeza viongozi wa Simba kwa kufanya usajili makini ambao umeweka uwiano sawa katika kila nafasi


"Nawapongeza sana viongozi wa Simba kwa kusajili wachezaji wazuri. Sasa nina vikosi viliwi vyenye uwiano sawa. Kama mchezaji mmoja anakosekana kwa sababu ya majeraha au yoyote, naweza kuweka mwingine pasipo kuathiri ubora wetu"


"Hili ni jambo muhimu sana kwa timu yenye malengo ya kushindania mataji. Tunawaheshimu wapinzani wote tutakaokutana nao lakini ifahamike malengo yetu ni kushinda mataji," alisema Robertinho


Msako wa mataji utaanza wiki ijayo kwenye Ngao ya Jamii ambapo August 10 Simba itacheza na Singida FG mchezo wa nusu fainali ambao utapigwa uwanja wa Mkwakwani


Robertinho na vijana wake wataanza kutoa burudani kwenye SIMBA DAY Jumapili ambapo Simba itacheza na Power Dynamo uwanja wa Benjamin MkapaAmbapo mechi itakuwa LIVE bure kwenye App yetu unaweza kuidownload Sasa bofya hapaDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz