Yanga kufunga usajili kibabe - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga kufunga usajili kibabe

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Keshokutwa Jumanne, Julai 18 Yanga inatarajiwa kumtangaza mchezaji ambaye usajili wake umekuwa gumzo kwa wiki kadhaa


Mchezaji huyo jina lake bado halijafahamika lakini jezi namba sita ambayo atakabidhiwa imepata umaarufu mkubwa na kuwafanya mashabiki kumsubiri kwa shauku kubwa


Jana katika uzinduzi wa wiki ya Mwananchi mkoani Mwanza, Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe alisema mchezaji huyo watamtangaza kwa utaratibu wa kipekee


Kamwe alibainisha kuwa nyota huyo na wenzake waliobaki, mpaka kufikia siku ya Jumanne watakuwa wametambulishwa wote


"Kama tulivyotangaza kuwa utambulisho wa wachezaji wetu umedhaminiwa na benki ya CRDB hivyo mchezaji namba sita atatambulishwa wa mwisho na tutazingatia haki za Mdhamini wetu"


"Bado hatujakamilisha utambulisho wa wachezaji wote, leo (jana) ilikuwa tutambulishe mchezaji mmoja hapa Mwanza lakini kutokana na changamoto za teknolojia tulikosa sceen kubwa ya kuweka hapa, bado hatujamaliza" alisema Kamwe


Yanga inatarajiwa kumtangaza mchezaji atakayekabidhiwa jezi namba sita usiku wa Jumanne (saa 6 na dakika 6) ambapo siku inayofuata atakuwa Makao Makuu ya benki ya CRDB


Wanachama na Mashabiki wa Yanga ambao watalipia kadi zao kupitia CRDB watapewa nafasi ya kupiga nae picha



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz