Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Wakati Simba ikiendelea na pre-season nchini Uturuki, winga Pape Ousmane Sakho yuko Senegal akisikilizia hatma yake
Inafahamika Sakho ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Simba, Wawakilishi wake waliwasilisha ombi kwa Simba ili aruhusiwe kuondoka baada ya kupata timu barani Ulaya
Kitendo cha Sakho kutorejea Tanzania kuungana na wenzake ni ishara kuwa msimu ujao hatakuwa sehemu ya kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi
Nafasi ya Sakho inatarajiwa kuchukuliwa na winga Luis Miquissone anayetua Msimbazi kwa mkopo wa msimu mzima akitokea Al Ahly
Simba inaweza kumsajili Miquissone moja kwa moja pale mkataba wake wa mkopo utakapomalizika
Sakho hakuwa na nafasi kwenye kikosi cha Kocha Robertinho Oliveira. Wasimamizi wake wamelazimisha mchezaji wao aondoke akajiunge na timu ambayo itamuhakikishia nafasi ya kucheza
No comments:
Post a Comment