Mayele mbioni kupewa mkono wa kwaheri na Yanga kuanzia sasa - EDUSPORTSTZ

Latest

Mayele mbioni kupewa mkono wa kwaheri na Yanga kuanzia sasa

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kuna asilimia ndogo kwa mshambuliaji Fiston Mayele kuendelea kuitumikia Yanga msimu ujao


Mfungaji bora huyo wa Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa 2022/23 pamoja na kombe la Shirikisho barani Afrika, anaweza kuibukia Misri kunako klabu ya Pyramids


Pyramids wamefikia mahitaji ya Yanga wakitajwa kuweka mezani dau la takribani Tsh Bil 2.8 pamoja na mshahara mnono kwa Mayele ambao ni mara mbili ya ule ambao Yanga walimuwekea ili kumuongezea mkataba


Mayele amebakisha mwaka mmoja tu katika mkataba wake, kama Yanga hautamuongezea mkataba au kumuuza sasa, msimu ujao ataondoka bure akiwa mchezaji huru


Mazingira haya yameiweka Yanga katika 'dilema' lakini ni wazi maamuzi ya mwisho lazima yazingatie  maslahi kwa pande zote mbili


Kinachosubiriwa sasa ni taarifa rasmi kuhusu mshambuliaji huyo kuuzwa lakini muhimu zaidi shauku kubwa ya Wananchi itakuwa kumfahamu mshambuaji atakayetua kuchukua nafasi yakeDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz