Yanga haijamaliza, MVP anashushwa leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga haijamaliza, MVP anashushwa leo

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema zoezi la utambulisho halijamalizika, leo wanashusha chuma kingine


Kamwe amedokeza kuwa mchezaji anayetangazwa leo ni mchezaji bora (MVP) katika ligi anayotokea 2022-23


"Baada ya kumtambulisha Waziri a burudani, bado hatujamaliza, leo tunashusha chuma kingine. Ni mchezaji bora zaidi katika ligi anayotoka"


"Usajili tuliofanya umezingatia mahitaji ya timu yetu, Wananchi wajiandae kupokea chuma kingine leo," alitamba Kamwe


Kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua kutoka Asec Mimosas ndiye Wananchi wanasubiri kuthibitisha utambulisho wake


Zouzoua ndiye mchezaji bora wa kikosi cha Asec Mimosas katika msimu uliopita lakini pia ndiye mchezaji bora (MVP) wa ligi kuu ya Ivory Coast


Ni kama ilivyokuwa kwa Stephane Aziz Ki, ambaye alitua Yanga msimu uliopita akiwa MVP wa Ivory Coast


Zouzoua anaweza kutumika kama kiungo mshambuliaji lakini pia anamudu kucheza kama kiungo wa ukabaji


Hivi karibuni alizawadiwa gari na Taasisi ya kiungo wa FC Barcelona Frank Kessie baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Asec Mimosas na ligi kuu ya Ivory Coast


Katika msimu uliopita Zouzoua alifunga mabao saba na kutoa pasi nne za mabaoDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz