Raja Casablanca ndo' basi tena Kimataifa msimu ujao - EDUSPORTSTZ

Latest

Raja Casablanca ndo' basi tena Kimataifa msimu ujao

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Miamba ya soka kutoka nchini Morocco Raja Casablanca hawatoshiriki michuano ya kimataifa msimu ujao baada ya kushindwa kufuzu kutokana na kiwango kibovu ilichokionyesha kwa msimu uliopita.


Raja imeshindwa kufuzu baada ya kumaliza nafasi ya tano kwenye Ligi Kuu nchini Morocco ikiwa na alama 44 ilizokusanya kwenye mechi 30.


Licha ya kiwango kibovu kwenye Ligi Raja ilikuwa na nafasi ya kufuzu michuano ya kimataifa kwa upande wa Shirikisho baada ya kufika fainali ya Kombe la Cup du Throne iliyocheza dhidi ya RS Berkane jana kwenye dimba la Prince Moulay Jijini Rabat nchini humo.


Matumaini yao yalikatishwa na penati ya beki wa kimataifa wa Burkina Faso ambaye alifunga penati ya Berkane kwenye 30 za ziada baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 0-0.


Msimu uliopita Raja ilishiriki Ligi ya Mabingwa na kuishia hatua ya robo fainali ilipotolewa na Al Ahly.


Kwenye hatua ya makundi ilifanikiwa kuongoza kundi C ambapo ilikuwepo Simba SC.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz