Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Nyanda wa Uhispania, David de Gea ametangaza kuondoka Manchester United na kuwaaga mashabiki na watumishi wa klabu hiyo kwa ujumla baada ya kuhudumu klabuni hapo kwa misimu 12.
Kupitia kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii De Gea ameandika "Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa upendo wa miaka 12 iliyopita. Tumefanikiwa mengi tangu mpendwa wangu Sir Alex Ferguson aliponileta kwenye klabu hii. Nilijivunia kwa namna ya ajabu kila nilipovaa shati hili.
“Umekuwa wakati usiosahaulika na wenye mafanikio tangu nilipokuja hapa. Sikufikiria kutoka Madrid nikiwa kijana mdogo tungefikia kile tulichofanya pamoja”
"Sasa, ni wakati muafaka wa kuchukua changamoto mpya, kujisukuma tena katika mazingira mapya.
“Manchester daima itakuwa moyoni mwangu, Manchester wamenitengeneza na hawataniacha kamwe.
De Gea (32) anaondoka klabuni hapo baada ya mkataba wake kufikia ukomo huku kukiwa na matumaini finyu ya kuongezewa mkataba mpya.
Mashetani wekundu kwa sasa wapo katika mchakato wa kutafuta mbadala wa De Gea huku golikipa wa Inter Milan, Mcameroon Andre Onana akiwa ukingoni kuchukua mikoba ya Mhispania huyo.
Post a Comment