Ahmed Ally aanza Tambo, awapiga mkwara wapinzani wa Simba - EDUSPORTSTZ

Latest

Ahmed Ally aanza Tambo, awapiga mkwara wapinzani wa Simba

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Meneja Habari wa Klabu ya Simba SC, Ahmed Ally ametamba na usajili ambao klabu hiyo imeufanya msimu huu na kudai kuwa kikosi chao kitawafunga mabao ya kutosha wapinzani wao pindi watakapokutana.


Ahmed amesema hayo mara baada ya kukamilisha usajili wa nyota kadhaa wa kimataifa wakiwemo Willy Onana, Kramo na Che Malone.


"Msimu ujao tutawafunga watu goli nyingi sana, iwe timu ndogo ama timu kubwa tumemfunga mtu goli chache ni magoli manne na hapo Phiri hajaamka vizuri, Baleke hajaamka vizuri, Ntibazonkiza hajaamka vizuri, Onana kichwa kinamuuma, Kramo ana mafua.


"Haiwezekani Phiri akukose, Kramo akukose, Baleke akukose, Chama akukose, Ntibazonkiza akukose, na Kibu Denis akukose. Halafu kuna vyuma vingine kama vitatu bado havijatua navyo vikukose aaaaaah," amesema Ahmed Ally.


Msimu uliopita SImba walimaliza msimu wakitoka kapa bila kombe huku wapinzani wao Yanga wakibeba makombe yote ya ndani kwa misimu miwili mfululizo.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz