Yanga, Mbeya City washushiwa rungu TFF - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga, Mbeya City washushiwa rungu TFF

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Klabu ya Mbeya City imetozwa faini ya Tsh laki tano (500,000) kwa kosa la watoto waokota mipira kuchelewa kwa makusudi kurejesha mipira kiwanjani kwenye mchezo wa sare ya 3-3 dhidi ya Yanga uwanja wa Sokoine.


Sambamba na hilo Mbeya City imetozwa faini Tsh milioni moja (1,000,000) kwa kosa la mashabiki wake kuwarushia chupa wachezaji wa Yanga wakati wakishangilia moja ya mabao waliyofunga.


Aidha klabu ya Yanga imetozwa faini ya Tsh milioni moja (1,000,000) kwa kosa la mashabiki wake kuwarushia chupa walinzi wa uwanjani kwenye mechi hiyo ambayo Yanga ililazimika kutoka nyuma 3-0 na kusawazisha magoli yote kunusuru alama moja kwenye sare ya 3-3.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz