Arsenal wathibitisha usajili wa Kai Havertz - EDUSPORTSTZ

Latest

Arsenal wathibitisha usajili wa Kai Havertz

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Klabu ya Arsenal imethibitisha kumsajili mshambuliaji Kai Havertz kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 65 kutoka Chelsea.


Havertz (24) raia wa Ujerumani amesaini mkataba wa kuwatumikia Washika mitutu hao mpaka Juni 2028 na atavaa jezi namba 29.


Kai anakuwa usajili wa kwanza wa Arsenal na anakuwa usajili wa pili ghali zaidi kwenye historia ya klabu hiyo nyuma ya Nicholas Pepe (pauni milioni 72).


Havertz ameondoka Chelsea baada ya kudumu nao kwa kipindi cha miaka mitatu tangu aliposajiliwa kwa ada ya pauni milioni 75 kutoka Bayer Leverkusen ya Ujerumani mnamo 2020.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz