Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Klabu ya Simba iko kwenye mazungumzo na TP Mazembe ili kumsajili mshambuliaji Jean Baleke moja kwa moja, imefahamika
Baleke alitua Simba kwa mkopo wa mwaka mmoja uliokuwa na kipengele cha kumsajili moja kwa moja kama Simba itaridhishwa na uwezo wake
Baleke ameitumikia Simba kwa miezi sita tu na muda huo umetosha kwa mabosi wa Simba kuchukua hatua ya kutaka kumsajili moja kwa moja
Habari njema ni kuwa Baleke mwenyewe amefurahia maisha ya Tanzania na hafikirii kurejea TP Mazembe hata pale muda wake wa mkopo utakapomalizika
Mkakati wa Simba msimu ujao ni kufanya vizuri katika mashindano yote watakayoshiriki, hilo litafanikiwa kama itakuwa na wachezaji bora kama Baleke
Post a Comment