Mbeya City yafuta viingilio mechi dhidi ya Mashujaa Fc - EDUSPORTSTZ

Latest

Mbeya City yafuta viingilio mechi dhidi ya Mashujaa Fc

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Zuber Homera amesema kuwa kuelekea mchezo wa marudiano kati ya Mbeya City dhidi ya Mashujaa hatua ya mtoano(play off) hakutakuwa na kiingilio ili kutoa nafasi kwa mashabiki kuingia kwa wingi uwanjani na kuipa hamasa timu yao


Homera amesema baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 3-1 na Mashujaa Fc katika mchezo wa kwanza wa play-off uliopigwa mkoani Kigoma,  wanapaswa kushikamana kipindi hiki ambacho Mbeya City inapatia mazingira magumu ya kupambana ili kusalia ligi kuu Tanzania bara


"Matokeo ya kule Kigoma sio mazuri,inapaswa tushirikiane kwa pamoja ili kuinusuru timu yetu, niwaombe sana mashabiki wa soka na wadau tufike kwa wingi uwanjani, hakutakuwa na kiingilio yaani bureee,tuujaze uwanja wa Sokoine ili tupindue matokeo," alisema Homera


Mchezo wa marudiano Kati ya Mbeya City dhidi ya Mashujaa hatua ya Play off umepangwa kuchezwa June 22, 2023 katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya


Mbeya City wanahitaji kupata ushindi wa goli 2-0 baada ya mchezo wa kwanza kupoteza kwa mabao 3 - 1 Lake Tanganyika Kigoma.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz