Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Uongozi wa klabu ya Simba SC, umetangaza kufikia makubaliano ya kuachana na kiungo mkabaji Victor Akpan, raia wa Nigeria.
Akpan alijiunga na Simba Julai, 2022 akitokea Coastal Union lakini baada ya uboreshaji mkubwa wa kikosi ambao Simba wamejinasibu kuufanya msimu huu, benchi la ufundi limeona hatakuwa sehemu ya mipango yao.
Simba imemshukuru Akpan kwa utumishi wake ndani ya timu na kumtakia kila lakheri kwenye maisha yake mapya ya soka nje ya Simba.
Simba wamesema wanaendelea kuboresha kikosi kuelekea msimu mpya wa Ligi 2023-24 na lengo lao wakisema ni kuwa na timu imara yenye ushindani itakayokuwa na uwezo wa kuchukua ubingwa.
No comments:
Post a Comment