Kauli ya Manara baada ya Nabi kufungasha virago Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Kauli ya Manara baada ya Nabi kufungasha virago Yanga

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Baada ya Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi kuondoka ndani ya klabu hiyo, Mhamasishaji wa Yanga, Haji Manara ameonyesha kusikitishwa na tukio hilo huku akidai kuwa hana neno la kusema zaidi ya kukubaliana na hali halisi.


@hajismanara; “Ipo hivyo Dunia nzima na kwa Watu wengi katika fani tofauti tofauti, kutafuta Changamoto mpya na kujaribu maisha sehemu nyingine ni jambo la kawaida na tumekuelewa Professor.


"Nenda ukijua umepata baraka zetu na always utabaki Mwananchi, nenda ukifahamu umeacha alama ndani ya mioyo yetu iliyo na mapenzi na wewe”


"Mataji Sita ndani ya Miaka miwili pamoja na fainali ya CAF ni ushahidi wa mema mengi kwetu, ni Mimi nilipoanza kukutambulisha kama Professor, huku mwanzoni ukikataa utambulisho huo, lakini jina likaenda kwa matokeo uliyokuwa unatupa siku hadi siku!”


“Tuseme nini zaidi ya kusema asante Nasruddin Mohammed Professor Nabi? Kila la kheri ktk maisha mapya nje ya Yanga”


NANI AIJUAE KESHO YAKE ?


NB: Makolo nasikia eti wamefurahia, uuh mkisikia Siku kaondoka Ghalib ndio pigeni Vigele gele.


Maisha ya Nasreddine Nabi tangia ajiunge na Yanga SC katika miaka yake miwili ya Maajabu.


Jumla ya Michezo 83 Jumla ya Michezo Aliyoshinda 57 Jumla ya Michezo Aliyopoteza 7 Jumla ya Michezo Aliyopata Sare 19 Jumla ya Makombe 6 Mechi 29 Za Ligi bila kufungwa 2021-22


Timu zilizopata ushindi katika utawala wa Nabi Azam FC Simba SC Ihefu FC Rivers United US Monastir USM Alger Al Hilal Omdurman.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz