Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Baada ya kuachana na Beno Kakolanya huku mlinda lango namba moja Aishi Manula akitarajiwa kuwa nje kwa miezi minne baada ya kufanyiwa upasuaji Afrika Kusini, Simba imelazimika kusajili mlinda lango mwingine
Caique mwenye umri wa miaka 25, akiwa amezaliwa Julai 31, 1997 katika mji wa Salvador huko Brazili kwa sasa anaichezea Ypiranga RS inayoshiriki Ligi ya Campeonato Brasileiro Serie C, sawa na First League hapa Tanzania akiwa kipa namba moja
Kipa huyo mwenye urefu wa futi 6 na inchi 5 alikulia kwenye akademi ya ES Victoria mwaka 2016, kabla ya kuitema na kwenda CSA ya Brazil sambamba na Ermis Aradippou ya Cyprus na Rochester NY ya Marekani kwa nyakati na misimu tofauti
Caique alikuwa kipa namba moja wa kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 (Brazil U-20), mwaka 2016 na 2017 kikishiriki michuano mbali mbali ya kimataifa kuonyesha kwamba ni mzoefu wa kutosha
Wakati akiwa kwenye kikosi hicho cha timu ya taifa alikuwa na nyota wengine wanaowika kwa sasa kwenye soka duniani wakiwemo Richarlison de Andrade wa Tottenham, Douglas Luiz wa Aston Villa, Lucas Paqueta wa West Ham na Gabriel Magalhes wa Arsenal
Awali Simba ilihusishwa kumuwania mlinda lango wa Al Hilal Issa Fofana lakini imekuwa ngumu kupata huduma yake baaada ya Al Hilal kugoma kumuuza
Post a Comment