Fei Toto: Asanteni Wananchi, bado naipenda Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Fei Toto: Asanteni Wananchi, bado naipenda Yanga

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Aliyekuwa mchezaji wa Yanga, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ amewashukuru mashabiki na viongozi wa Yanga kwa kipindi chote ambacho amefanya kazi katika klabu hiyo.


Fei Toto ametoa shukrani hizo mara baada ya kujiunga na Klabu ya Azam akitokea Yanga ambayo ameitumikia tangu mwaka 2018.


“Namshukuru kwa kufikia wakati huu, pia ninamshukuru sana Mhe. Rais Samia kwa kufanikisha kumaliza hili jambo hili, ninamuombea kwa Mungu ambariki na amjalie kila la kheri.


“Ninawashukuru mashabiki na viongozi wa Yanga kwa kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja, ninawatakia kila la kheri. Mimi bado naipenda Yanga na mashabiki pia bado nawapenda, asanteni sana,” amesema Fei Toto.


Fei Toto amesaini mkataba wa miaka mitatu kuwatumikia Wauza Ukwaju wa Dar, baada ya kumaliza sakata lake la kimkataba na na Mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz