Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Tofauti na msimu uliopita, Mzunguumo mmoja kabla Ligi Kuu Tanzania Bara kumalizika, vita imehamia katika timu zinazopigana kuepuka kucheza mechi za mchujo ‘Play Off’, huku sehemu zote zilizobaki kila timu ikivuna ilichopanda.
Baada ya mechi zilizochezwa juzi Jumanne (Juni 06), rasmi Polisi Tanzania imeungana na Ruvu Shooting kushuka daraja, bingwa akiwa ni Young Africans huku pia wawakilishi wa Tanzania Bara katika michuano ya kimataifa, timu nne zimejulikana.
Macho na masikio ya mashabiki sasa kesho Ijumaa (Juni 09) ili kufahamu timu zipi zitaangukia kucheza mechi za mchujo ‘Play Off’ dhidi ya timu za Ligi ya Championship, Mashujaa FC ya Kigoma.
Timu tano ambazo ni KMC, Mbeya City, Coastal Union, Mtibwa Sugar na Dodoma Jiji zinaonekana zipo katika hatari zaidi ya kwenda kucheza ‘Play Off’ kutokana na nafasi zao kwenye msimamo wa ligi.
KMC itakuwa ugenini kucheza dhidi ya Mbeya City, Mtibwa Sugar watawakaribisha Geita Gold, Dodoma Jiji itacheza dhidi ya Ruvu Shooting, na Coastal Union itakuwa Azam Complex kuwakabili Simba SC.
Chanzo: Dar24
Post a Comment