Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kiungo mpya wa Azam FC, Feisal Salum "Fei Toto" amezima minong'ono iliyokuwa ikiendelea mitandaoni kuhusu michango aliyokuwa akichangiwa kwa lengo la kupata fedha na kwenda kufungua kesi katika Mahakama ya usuluhishi wa Michezo CAS akitaka kuvunja Mkataba na Klabu ya Yanga.
Sakata hilo sasa limekwisha na tayari Kiungo huyo ameuzwa kwa Klabu ya Azam FC na amesaini Mkataba wa Miaka mitatu unaotamatika waka 2026.
Akizungumza wakati akitambulishwa katika Makao Makuu ya Azam FC "Mzizima" Feisal amesema;
"Kwanza nimshukuru Mwenyezi mungu kwa kuniwezesha kulimaliza suala hili, vilevile nimshukuru Mh Rais kwa kulifanya wepesi suala hili hali kadhalika na viongozi wa Yanga"
"Kuhusu michango wengi mitandaoni wamekuwa wakiuliza inakuaje, kwanza napenda kuwashukuru kwa moyo wao lakini niseme tu waliochanga ni wengi na siwezi kuwafahamu kwa sababu pesa zimetoka maeneo tofauti tofauti"
"Ninachoweza kusema ni kuwa sitarudisha pesa kwa kila aliechanga ila nitazipeleka kwa watoto yatima msikitini na kanisani na nafikiri zitakuwa zimekwenda mahala sahihi inshallah" amemaliza Feisal
Post a Comment