Rais Samia awapa Yanga "Maua yao" ushindi dhidi ya Marumo - EDUSPORTSTZ

Latest

Rais Samia awapa Yanga "Maua yao" ushindi dhidi ya Marumo

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza klabu ya Yanga SC kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.


“Hongereni Yanga kwa ushindi katika mchezo wenu wa raundi ya kwanza ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup)”.


“Nawatakia maandalizi mema kwa mchezo wenu wa raundi ya pili, muendelee kuiheshimisha nchi yetu. Hamasa yangu inaendelea,” amesema Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.


Mabao ya Yanga jana yalifungwa na viungo, Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 64 na Mghana Bernard Morrison dakika ya 90 na ushei na sasa wanatakiwa kwenda kuulinda ushindi huo kwenye mchezo wa marudiano Mei 17 Uwanja wa Royal Bafokeng, Phokeng, NW.


Wakiitoa Marumo, Yanga watakutana na mshindi wa jumla kati ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast na USM Alger ya Algeria katika Fainali zitakazopigwa Mei 28 na Juni 3.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz