Hitimana kuibukia Jkt Tanzania - EDUSPORTSTZ

Latest

Hitimana kuibukia Jkt Tanzania

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Baada ya kufanikiwa kurejesha timu Ligi Kuu Tanzania Bara kuelekea msimu mpya wa 2023/24, uongozi wa Klabu ya JKT Tanzania upo katika mchakato wa kumpa ajira, aliyekuwa Kocha Mkuu wa KMC FC, Thierry Hitimana, kukinoa kikosi hicho kwa msimu ujao, imefahamika


Licha ya uongozi wa JKT Tanzania kutoweka wazi suala hilo huku wakidai kuwa wataendelea na Kocha Hamsini Malale aliyeipandisha timu hiyo Ligi Kuu endapo anahitaji kuendelea kubaki katika timu hiyo, lakini taarifa za ndani zimedokeza kuwa klabu hiyo ipo katika mazungumzo na Hitimana.


Hata hivyo, Malale alipoulizwa juu ya mustakbali wake juu ya maboresho ya kikosi chake, alisema hawezi kuweka mipango yake ya usajili ya msimu ujao kwa sababu hajui hatima yake.


Alipotafutwa Hitimana mwenyewe akagoma kuweka wazi dili hilo akisisitiza kuwa hakuna timu iliyomfuata


"Hakuna kiongozi aliyenifuata kwa ajili ya mazungumzo yoyote, hilo suala kama lipo, kwangu ni vizuri kwa sababu hakuna mtu anayekataa kazi anapoipata," alisema Hitimana


Hitimana ni kocha mwenye uzoefu wa Ligi kuu ya Tanzania Bara akiwa amewahi kuzifundisha Namungo Fc na Simba kabla ya kujiunga na KMCDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz