Yaliyojiri Tff Leo kwenye kesi ya Feisal Toto na Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Yaliyojiri Tff Leo kwenye kesi ya Feisal Toto na Yanga

Kupata Kifurushi cha bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mkurugenzi wa Sheria klabu ya Yanga Simon Patrick amesema msimamo wa klabu kuhusu mchezaji Feisal Salum haujabadilika na kuwa walishafungua milango kwa mchezaji huyo kufuata taratibu kama anataka kuondoka

Leo Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana kujadili maombi ya Feisal kwa Kamati hiyo akiomba mkataba wake na klabu ya Yanga uvunjwe

Simon aliiwakilisha Yanga kwenye shauri hilo ambalo hata hivyo halikusikilizwa baada ya upande wa Feisal kushindwa kutimiza baadhi ya matakwa ya kisheria. Shauri hilo limepangwa kusikilizwa tena May 04 mwaka huu

Akizungumza na Wanahabari muda mfupi baada ya kutoka kwenye Kikao cha Kamati, Simon alisema Yanga haina pingamizi kwa Feisal kuondoka anachopaswa kufanya ni kufuata utaratibu ambao unafahamika

"Nafikiri tulishaweka wazi msimamo wetu kupitia taarifa tuliyoitoa huko nyuma. Hatuna pingamizi lolote juu ya mahitaji ya Feisal"

"Anayemuhitaji Feisal aje klabuni au yeye akitaka kuondoka aje klabuni utaratibu anaujua tupeane mkono wa kwaheri," amesema SimonDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz