Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Doumbia aliingia dakika ya 67 kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 katika uwanja wa Azam Complex
Doumbia alitumia takribani dakika 25 alizotumika katika mchezo huo akionyesha umahiri wake katika kupiga pasi, kunusa na kuokoa hatari pamoja na kucheza mipira ya juu
Mara kadhaa Nabi aliweka bayana kuwa Doumbia hatumiki sio kwa sababu ni mchezaji mbaya, bali anampa muda ili aweze kuzoea mbinu ya aina ya uchezaji wa wenzake
Wakati Doumbia anasajiliwa na Yanga, tayari aliwakuta wenzake wanafanya vizuri katika nafasi anayocheza hivyo ilikuwa ni lazima kwa Nabi kuwa na uvumilivu ili kuhakikisha hamuweki kwenye presha kubwa
Taratibu Doumbia ameanza kuonekana na bila shaka wale waliokuwa na mashaka nae watatulia..!
Post a Comment