wachezaji wa Simba wadaiwa kugomea mechi ya Wydad - EDUSPORTSTZ

Latest

wachezaji wa Simba wadaiwa kugomea mechi ya Wydad

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kwa mujibu wa taarifa ni inadaiwa kuwa wachezaji wa klabu ya Simba wamefanya mgomo kuelekea mchezo wao wa kwanza wa robo fainali ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Wydad jumamosi hii, mchezo ambao utapigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa.


Taarifa zinasema kua wachezaji hao wamegoma kwasababu ya kutokulipwa bonasi zao za mechi nne (4) za ligi pamoja na zile walizoahidiwa katika mchezo wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Horoya.


Katika mchezo dhidi ya Yanga walipewa ahadi ya bonasi kama wakishinda mchezo huo kitu ambacho kilitekelezwa lakini walipewa zikiwa zimekatwa katwa jambo ambalo wachezaji hawakulipenda.


Huenda leo Rais wa heshima wa klabu ya Simba akafanya kikao na wachezaji hao juu ya hiki kilichotokea.


Bado haijathibitikia kama taarifa hizi ni za kweli ama ni propaganda kuelekea mcheszo huo mgumu na muhimu kwa Simba SC.


Chanzo: Edgar KibwanaDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz