VIDEO: Mwanasarakasi Afariki Wakati wa Onyesho na Mumewe. - EDUSPORTSTZ

Latest

VIDEO: Mwanasarakasi Afariki Wakati wa Onyesho na Mumewe.

 

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


Mwanasarakasi huko nchini China amefariki dunia wakati wa onyesho lake mubashara la angani, hali iliyozua hofu na vilio kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ukosefu wa hatua za usalama.

Mwanamke huyo aliyepewa jina la Sun, alianguka jukwaani alipokuwa akifanya mazoezi ya angani siku ya Jumamosi na mumewe katika kijiji karibu na mji wa Suzhou katikati mwa mkoa wa Anhui na alipelekwa hospitalini lakini alifariki kutokana na majeraha, serikali ya wilaya ya Tongqiao ilisema katika taarifa Jumatatu.

Picha za mtandaoni za tukio hilo zilionyesha wanandoa hao wakivutwa hewani na kreni juu ya jukwaa kubwa la nje, huku mwanamke huyo akiwa amemshikilia mumewe ambaye mikono yake ilikuwa imefungwa kwenye vipande viwili vya kitambaa vinavyoning’inia kutoka kwenye kreni hiyo.

Walipokuwa wakiyumba angani, mwanamke huyo alizungusha mikono yake kichwani mwa mumewe na kumning’iniza wakati wa harakati ya kupishana lakini alishindwa kushikilia sehemu ya kitambaa vizuri na kisha kuanguka huku kukiwa na mayowe kutoka kwenye umati uliokuwa umewazunguka.Juhudi za mumewe hazikuzaa matunda kwani alijaribu kumshika kwa miguu yake lakini akashindwa, picha zilionyesha.

Video za wakati huo wa kutisha zilishtua mitandao ya kijamii ya Uchina na watumiaji wengi wa mitandao walihoji kwa nini mwanamke huyo hakuvaa mkanda wowote wa usalama, na kwa nini hapakuwa na wavu wa usalama na Wengine walitaka sheria kali zaidi kuhusu tasnia ya sarakasi na ulinzi bora kwa wasanii.


“Aina hii ya uchezaji sarakasi ya katikati ya anga ni hatari sana angalau weka wavu wa usalama chini ili (mchezaji) aweze kulindwa dhidi ya kuanguka,” maoni kwenye jukwaa la China la Weibo kutoka ukurasa wa Twitter.

“Hata waigizaji wawe na ujuzi gani, daima kutakuwa na makosa. Inakuwaje hakuna hatua za usalama?”
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz