Mechi ya Simba vs Yanga yaingiza mamilioni - EDUSPORTSTZ

Latest

Mechi ya Simba vs Yanga yaingiza mamilioni

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Taarifa kutoka TFF imeeleza kuwa, mchezo wa dabi ya Simba SC dhidi ya Yanga SC imeingiza mapato ya shilingi Mil. 410,645,000.


Katika mchezo huo, jumla ya mashabiki 53,569 waliingia ambapo VIP waliingia watazamaji 340 kwa kiingillio ch shilingi 30,000 na kupatikana jumla y ash 10,200,000, VIP B waliingia watazamaji 4160 kwa kiingilio cha shilingi 20,000 ikapatikana jumla ya sh 83,200,000.


VIP C waliingia watazamaji 2,004 kwa kiingilio cha sh. 15,000 na kupatikana sh. 30,060,000 wakati jukwaa la rangi ya machungwa waliingia watazamaji 10,372 kwa kiingilio cha sh 10,000 na kupatikana sh. 103,720,000 na jukwaa la mzunguko waliingia watazamaji 36,693 kwa kiingilio cha 5000 na kupatikana sh 183,465,000.


TFF imetoa mgawanyo wa mapato hayo ambapo timu mwenyeji imepata sh 188,987,181.10 huku fedha zingine zikienda kwenye kodi, BMT na vitu vingine.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz