Tetesi za usajili barani ulaya Leo Jumamosi - EDUSPORTSTZ

Latest

Tetesi za usajili barani ulaya Leo Jumamosi

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Chelsea wako tayari kumfanya kiungo wa kati wa Barcelona na Uhispania Gavi kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa pesa nyingi kwenye Premier League ili kumsajili kinda huyo mwenye umri wa miaka 18. (AS - in Spanish)


The Blues pia wana imani kuwa wanaweza kushinda mbio za kumnunua mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 24, hata bila ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao. (90min)


Liverpool wamemfanya mchezaji wa kimataifa wa Argentina wa Brighton Alexis Mac Allister, 24, kuwa mlengwa wao mkuu kama kiungo wa kati msimu huu. (Football Insider)


Mshambulizi wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 30, anatazamiwa kukataa kuhamia Saudi Arabia na kusalia Ulaya mara tu atakapokuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu. (Evening Standard)


Mshambulizi wa Uingereza Harry Kane, 29, atasubiri kutathmini mkataba mpya katika klabu ya Tottenham mara tu klabu hiyo itakapomteua meneja mpya, huku Manchester United na Bayern Munich zikiwa na nia ya kumsajili. (90min)


Manchester City na Liverpool wanamtazama mlinzi wa Chelsea Mwingereza mwenye umri wa miaka 20 Levi Colwill, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Brighton. (Standard)


Mbali na Colwill, Liverpool pia wanavutiwa na viungo wa Chelsea wa Uingereza Conor Gallagher, 23, na Mason Mount, 24. (Football Insider) Lakini Chelsea wanatarajiwa kufanya msukumo wa mwisho kumshawishi Mount kusaini mkataba mpya. (ESPN)


The Blues wamefanya mazungumzo na Ruben Amorim wa Sporting Lisbon, 38, huku msako wa klabu hiyo wa kutafuta meneja mpya wa kudumu ukiendelea. (Guardian)


Barcelona wanakaribia kufikia makubaliano na nahodha wa Manchester City na kiungo wa kati wa Ujerumani Ilkay Gundogan, 32. (90min) Manchester City ni miongoni mwa vilabu vinavyomfuatilia winga wa Portsmouth Koby Mottoh mwenye umri wa miaka 16. (Football Insider)


Chelsea inaweza kuuza wachezaji tisa wa kikosi cha kwanza ili kusawazisha fedha zao, huku mshambuliaji wa Marekani Christian Pulisic, 24, akiwa kati ya wale ambao wanaweza kuondoka. (Mirror)


Roma wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Brazil Roberto Firmino, 31, mkataba wake na Liverpool utakapokamilika msimu huu. (Nicolo Schira)


Roma pia wanafikiria kumsajili beki wa pembeni wa Leicester City na England James Justin, 25, kwa mkopo na chaguo la kufanya uhamisho huo kuwa wa kudumu kwa ada ya euro 20m (£17.7m). (Calciomercato - in Italian)


Liverpool ni miongoni mwa vilabu kadhaa vinavyomfuatilia winga wa Lyon na Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 Bradley Barcola, 20. (Fabrizio Romano)


Fulham itaweka bei ya pauni milioni 60 kwa kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha, 27, ambaye analengwa na Manchester United. (Metro)


BBCDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz