Meneja wa Baleke amaliza utata "Ni mchezaji wa TP Mazembe" - EDUSPORTSTZ

Latest

Meneja wa Baleke amaliza utata "Ni mchezaji wa TP Mazembe"

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Meneja wa mshambuliaji kinara wa Simba, Jean Othor Baleke raia wa Congo DR, Clovis Mashisha amekiri kuwa mchezaji huyo ana mkataba na Klabu ya TP Mazembe hivyo yuko Simba kwa Mkopo.


Mashisha amesema hayo wakati akifanyiwa mahojiano maalum na chombo kimoja cha Habari nchini Tanzania baada ya tetesi kusambaa kuwa Baleke si mchezaji wa Simba badala yake yupo klabuni hapo kwa mkopo na muda wowote Mazembe wanaweza kumchukua mchezaji wao.


“Ni kweli baleke yupo Simba kwa mkop. Baleke na Mazembe wana mkataba wa miaka mitano, ameshafanya kazi miaka miwili kwa hiyo bado miaka mitatu. Kwenye mkataba wa Simba na Baleke ni wa miaka miwili, yaani ni mkopo wa miaka miwili.


“Mazembe walikuwa wagumu kumwachia Baleke kwa sababu hawakuwa na starika, lakini cha pili walikuwa na ofa ya kumuuza Misri lakini yeye hakutaka kwa sababu alikuwa ameshagomba na viongozi wa Mazembe na mazoezini alikuwa haendi, wakaona bora wamwachie aende sehemua ambayo yeye anapenda.


“Lakini namna ambavyo kazi tumeifanya mpaka dakika hii, Baleke na Mazembe watakuwa wanabakisha mwaka mmoja, sasa tutajitahidi tuifanyie kazi mapemba ili Baleke abakie Simba.


“Mchezaji anapocheza anafunga, anakuwa na furaha na anapata mafanikio ndiyo sehemu sahihi kwake. Huwezi kupeleka mchezaji sehemu akawa hafanyi vizuri maana yake hiyo siyo seheme sahihi kwake. Baleke ameonyesha uwezo mzuri kwa hiyo ninaona Simba yupo sehemu sahihi kabisa kwake.


“Baleke anakaa vizuri na wachezaji wenzake, ameniambia anaongea vizuri na Saido, Chama na wachezaji wengine, wanaishi vizuri sana, furaha ipo licha ya changamoto kidogo ambazo huwa hazikosi sehemu yoyote,” amesema Mashisha.


Baleke aliyesajiliwa na Simba kwa mkopo katika dirisha dogo la usajili msimu huu, tayari ameshacheza mechi 14 na kufunga mabao 14 kwenye michezo mbalimbali ya kimashindano, jambo ambalo limewafanya viongozi na mashabiki wa timu hiyo kumuamini na kuamini kuwa wametibu tatizo la safu ya ushambuliaji lilikokuwa likiwasumbua tangu kuondoka kwa Meddie Kagere na Chris Mugalu.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz