Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mabingwa wa England na Ujerumani watakutana uwanjani Etihad siku ya Jumanne, wakati Manchester City wakiwakaribisha Bayern Munich katika mkondo wa kwanza wa robo fainali ya UEFA Champions League
Huku timu zote zikitakata kwene michuano hiyo, zimekabiliana na upinzani mkali kwenye ligi ya nyumbani
Man City iliifunga Southampton mabao 4-1 mwishoni mwa juma na kuendelea kuchuana na Arsenal katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza
Huo ulikuwa ushindi wao wa nane mfululizo. Mabao mengine manne mwishoni mwa juma yanamaanisha kuwa wamezifumania nyavu mara 31 katika kipindi hiki cha ushindi wa michezo minane.
Huku Erling Haaland akiwa kinara wa ufungaji, ana mabao 10 katika mechi sita tu za Ligi ya Mabingwa msimu huu, lakini Haaland hajawahi kufurahia mafanikio dhidi ya Bayern, ikipoteza mechi zote saba wakati akiwa na Borussia Dortmund.
Haaland alikuwa na mchango mkubwa kwa Man City katika kuwaona wakiendelea hadi hatua hii ya robo fainali, akifunga mabao matano katika kipigo kikubwa cha 7-0 dhidi ya RB Leipzig, na kuthibitisha ushindi wa jumla wa 8-1 katika hatua ya 16 bora.
City walikutana na Bayern mara kadhaa katika miaka ya karibuni katika Ligi ya Mabingwa, wakishinda mara mbili kati ya mechi tatu walizokutana Etihad, huku kichapo chao pekee kwenye ardhi ya nyumbani kikiwa ni wakati Pep Guardiola alipokuwa ugenini na wababe hao wa Ujerumani
Licha ya kukaa kileleni mwa Bundesliga, Bayern hawako imara zaidi kama walivyo City nyumbani, pamoja na Thomas Tuchel kuanza vyema majukumu yake katika klabu hiyo akiirejesha kileleni mwa Bundesliga
Mechi ya kwanza ya Tuchel ilishuhudia Bayern wakiwashinda wapinzani wao wa taji Dortmund katika Uwanja wa Allianz Arena, lakini wakafuatia kwa kushindwa kwa mshtuko dhidi ya Freiburg, na kuondoshwa katika DFB-Pokal katika hatua ya robo fainali.
Wakarejesha ari ya ushindi wikiendi iliyopita na kujiimarisha kileleni mwa Bundesliga kwa tofauti ya alama mbili
Bayern wanalitaka taji la Ligi ya Mabingwa msimu huu, Tuchel aliisaidia Chelsea kushinda taji hilo mbele ya Manchester City msimu mmoja nyuma
Je atafanikiwa kuwaondosha tena kwenye michuano hiyo?
Post a Comment