Matchday Live: Yanga vs Kagera sugar - EDUSPORTSTZ

Latest

Matchday Live: Yanga vs Kagera sugar

Kupata Kifurushi cha bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Mabingwa watetezi Ligi Kuu ya NBC, Yanga leo wako uwanjani kuikabili Kagera Sugar katika mchezo wa ligi hiyo raundi ya 25


Mchezo huo wa kiporo utapigwa saa 1 usiku katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi


Wakati Ligi ikielekea ukingoni, Yanga inasaka alama tisa kutoka kwenye mechi sita zilizosalia ili kujihakikishia ubingwa wa 29


Ushindi dhidi ya Kagera Sugar utawafanya wazidi kukaribia taji la pili mfululizo


Ni wazi mchezo huo hautakuwa mwepesi kutokana na ubora wa Kagera Sugar hasa wanapokutana na Yanga


Jana katika Mkutano na Wanahabari, Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze alikiri Kagera Sugar waliwapa wakati mgumu kwenye mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba ingawa walishinda bao 1-0


Kaze alisema leo wanahitaji kuwa katika ubora wao ili kuweza kushinda mchezo huo


Habari njema kwa Yanga ni kuwa kwa sasa hawana changamoto kubwa ya wachezaji majeruhi, Aboutwalib Mshery ndiye mchezaji pekee anayekosekana


Yanga inahitaji kushinda ili kurejesha gap la alama nane dhidi ya watani zao Simba ambao jana walipata ushindi dhidi ya Ihefu Fc na kufikisha alama 60


Matokeo tofauti na ushindi ni wazi yatawaongezea presha kuelekea dabi ya Kariakoo itakayopigwa Jumapili, April 16 2023 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Mechi Itakuwa LIVE kwenye App yetu bofya hapa kuidownload sasa ili uweze kuitazama mechi hii LIVE kupitia simu YakoDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz