Nabi arudi na mkakati huu kuhusu Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Nabi arudi na mkakati huu kuhusu Yanga

Kupata Kifurushi cha bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema wanahitaji kupambana katika mechi zinazokuja mbeleni ili kuhakikisha wanafikia malengo


Nabi aliwasili nchini jana mchana akitokea Tunisia kushughulikia masuala ya kifamilia


Nabi amesema kuna kazi kubwa iko mbele yao katika mechi zinazofuata na amewapa maelekezo wachezaji wake kuhakikisha wanaongeza bidii ili kufanikisha malengo yao


"Tuna ratiba ngumu mbele ikiwa ni pamoja na mechi ambazo zinaweza kuamua hatma yetu ya ubingwa wa Ligi Kuu na michuano ya Kimataifa ya CAF. Nimezungumza na wachezaji ni lazima waongeze bidii ili tuweze kutimiza malengo yetu," Nabi aliiambia Yanga Media


Nabi amerejea wakati mwafaka wakati kikosi chake kikikabiliwa na mechi muhimu za ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar na Simba


Jumanne April 11 Yanga itacheza na Kagera Sugar uwanja wa Azam Complex kisha kufuatiwa na mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili, April 16 katika uwanja wa Benjamin Mkapa


Yanga itakuwa katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa kama itashinda mechi hizo


Mchezo wa kwanza wa robo fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rivers United utapigwa April 23 nchini Nigeria na marudiano kupigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, April 30



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz