Karim Benzema apiga Hat trick ndani ya dakika 7 - EDUSPORTSTZ

Latest

Karim Benzema apiga Hat trick ndani ya dakika 7

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Karim Benzema alifunga hat-trick ndani ya dakika ya saba Real Madrid ilipoilaza Real Valladolid 6-0 Jumapili kwenye La Liga


Mabingwa Real Madrid, wa pili, wako nyuma kwa pointi 12 nyuma ya vinara Barcelona baada ya Wakatalunya hao kuwalaza Elche mabao 4-0 siku ya Jumamosi, zikiwa zimesalia mechi 11 kila moja.


Kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya nne bora kiliongezeka huku Villarreal, iliyo nafasi ya sita, ikiishinda Real Sociedad inayoshika nafasi ya nne 2-0, na Atletico Madrid kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Betis katika nafasi ya tano


Madrid inayonolewa Carlo Ancelotti ni kama ilikuwa ikifanya mazoezi kwa pambano lao la nusu fainali ya Copa del Rey siku ya Jumatano na mahasimu wao wakubwa Barcelona wakiwasambaratisha Valladolid, wa 16 na pointi moja juu ya eneo la kushuka.


Rodrygo Goes alifunga bao la kwanza mapema, kabla ya Hat-trick ya Benzema, huku Marco Asensio akifunga la tano katika kipindi cha pili na Lucas Vazquez akiongeza jingine baadaye


"Karim ni mchezaji wa kuvutia, nyota wa kiwango cha dunia, amekuwa hapa miaka 14 na mwaka baada ya mwaka anafunga mabao," Vazquez aliiambia DAZN


"Mwaka baada ya mwaka amekuwa nambari tisa wa Madrid, hakuna mengi ya kusema juu yake, nina furaha sana kwake na kufurahia kucheza naye katika kila mchezo"



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz