Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Licha ya kuyumba kidogo tofauti na walivyoanza msimu huu kwenye ligi kuu, Azam Fc leo wana nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Mtibwa Sugar
Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi saa 1 usiku
Kwa Azam Fc kombe la FA sasa ni muhimu zaidi kwao ili kujihakikishia kushiriki michuano ya CAF msimu ujao
Kwenye Ligi Kuu wanashika nafasi ya nne nyuma ya Yanga, Simba na Singida Big Stars
Msimu ujao Tanzania itatoa timu nne kwenye michuano ya CAF ambapo mshindi wa kwanza na pili katika ligi kuu watacheza ligi ya mabingwa wakati mshindi wa tatu na bingwa wa kombe la FA watacheza kombe la Shirikisho
Kama itatokea bingwa wa FA ni timu iliyomaliza nafasi ya kwanza au pili kwenye ligi kuu, timu itakayoshika nafasi ya nne kwenye ligi itakwenda Shirikisho
Azam Fc wanakutana na Mtibwa Sugar ambayo msimu huu imekuwa haitabiriki. Timu hizo zilipokutana kwenye ligi uwanja wa Manungu, Azam Fc iliibuka na ushindi wa mabao 4-3
Baada ya mechi ya FA, timu hizo zitachuana tena katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa hapohapo kwenye uwanja wa Azam Complex, April 15
No comments:
Post a Comment