Hakuna kiongozi au Mwanasimba anayetaka kuwaona Young Africans wakitangaza ubingwa dhidi yetu" Ahmed - EDUSPORTSTZ

Latest

Hakuna kiongozi au Mwanasimba anayetaka kuwaona Young Africans wakitangaza ubingwa dhidi yetu" Ahmed

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Katika kuhakikisha wanashinda mchezo wa Jumapili (April 16) dhidi ya Young Africans, baadhi ya viongozi Klabu ya Simba SC kutoka kamati mbalimbali wamehamishia shughuli zao kambini ili kujihakishia ushindi.


Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, Young Africans na Simba zilitika sare ya bao 1-1. Na sasa Young Africans kileleni mwa ligi ikiwa na alama 68 mbele ya Simba wenye alama 60 tu.


Taarifa kutoka Simba SC zimeeleza kuwa, tangu kikosi hicho kimeingia kambini huko Mbweni baadhi ya viongozi wamekuwa wakishinda huko na kutoka usiku mnene ili kuhakikisha wanawatia moyo na nguvu wachezaji wao.


“Kiukweli tangu tuingie kambini kuna baadhi ya viongozi wamekuwa hawaishi mazoezini na kambini nadhani lengo ni kuendelea kutoa hamasa kwa ajili ya mechi yetu ijayo ambayo kila kiongozi anatutaka tuifunge Yanga,” zimeeleza taarifa hizo


Kwa upande wa Meneja Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema: “Ukubwa na umuhimu wa mchezo huu kwetu ni lazima tushikamane maana tunahitaji kuifunga Young Africans tu.”


“Hakuna kiongozi au Mwanasimba anayetaka kuwaona Young Africans wakitangaza ubingwa dhidi yetu, hivyo tumejipanga kuvuna ushindi bila kujali staili tutakayoitumia maana hatujawafunga muda na sasa heshima yetu pekee ni kuwapa kichapo.”Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz