Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kiungo Ismael Sawadogo Jumatatu ya wiki hii alirejea uwanjani kwenye mechi ya Simba na Ihefu, lakini akatolewa baada ya dakika 26 na kuibua mijadala mtandaoni, ila mchezaji huyo amefunguka kuwa ataendelea kuipambania timu yake kila atakapopata nafasi
Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Higland Estate, jijini Mbeya Simba ilishinda mabao 2-0 yote yakifungwa na straika hatari, Jean Baleke.
Sawadogo alisajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Difaa El Jadida ya Morocco, amekuwa na mwanzo usioridhisha katika kikosi cha Simba
Nyota huyo raia wa Burkina Faso amesema kutolewa uwanjani mapema ni jambo la kawaida na kuwa haliwezi kumuondolea malengo yake
"Siwezi kutoka mchezoni naelewa kutolewa kikosini ni kawaida mimi sio wa kwanza kutolewa mapema naelewa hilo na haliniondoi kuwa nina uwezo wa kucheza nahitaji muda zaidi ili kuweza kuonyesha uwezo wangu"
"Niliondolewa labda sikufiti kile kocha alikuwa anatamani kuona nikikifanya, lakini najiamini na natamani kupewa nafasi ya kucheza ili niweze kuonyesha uwezo wangu," alisema Sawadogo
Sawadogo amesema bado ni mapema kwake kuzungumza kama ligi ni ngumu kwa sababu hajapata muda wakutosha kucheza lakini jambo muhimu ni kuona SImba inapata matokeo mazuri
"Sijapata nafasi ya kucheza michezo mingi lakini nimekuwa nikifuatilia ni ligi nzuri iliyo na ushindani lakini siwezi kuelezea changamoto zake kwasababu sipati nafasi ya kucheza ninachofurahia timu inapata matokeo na natamani kupata muda wa kucheza ili kuonyesha kile nilichonacho," Sawadogo alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti
Post a Comment