Yanga yafukuzia Rekodi hii - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga yafukuzia Rekodi hii

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Kwa sasa mashabiki wa Yanga wana raha ya aina yake baada ya kuishuhudia timu yao ikitinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika


Wananchi wanaona kabisa ni msimu ambao huenda wakaenda kushuhudia kupatikana mafanikio makubwa katika klabu yao kwenye miaka ya hivi karibuni


Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema baada ya kufanikiwa kutinga robo fainali ya kombe la Shirikisho, malengo sasa ni kuitafuta nusu fainali, fainali na hata kusaka taji la kwanza barani Afrika kwani inawezekana


Wakati bendera ya Kimataifa ikiendelea kupepea vyema, Yanga pia imedhamiria kutetea mataji yake yote ya ndani


Ngao ya Jamii tayari iko mikononi, dalili njema zinaonekana kwenye ligi kuu, Yanga ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama nane huku zikiwa zimesalia mechi sita kuhitimisha msimu


Kimahesabu Yanga inahitaji kushinda mechi tatu zinazofuata ili kutetea ubingwa. Kama Wananchi watashinda mehci dhidi ya Kagera Sugar, Simba na Singida Big Stars basi hesabu zitakamilika mapema tu


Lakini iwapo itatokea watani zao Simba watashindwa kupata ushindi katika mechi zao zinazofuata kazi itakuwa rahisi zaidi


Kwenye kombe la FA Wananchi wako hatua ya robo fainali wakitarajiwa kuchuana na Geita Gold


Kama hesabu zitakwenda sawa, Yanga inaweza kufunga msimu ikiwa na mataji manne na kufanya msimu huu kuingia katika kumbukumbu ya klabuDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz