Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Adel Amrouche amewaongeza walinzi wawili wa Simba Shomari Kapombe na Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' katika kikosi cha timu ya Taifa
Rais wa TFF Wallace Karia amesema Amrouche amewahitaji wachezaji hao kuongeza nguvu kwenye kikosi chake kuelekea mchezo wa marudiano kuwania kufuzu Afcon 2023 dhidi ya Uganda siku ya Jumanne Machi 28, 2023
"Mwalimu amewaongeza kwenye kikosi wachezaji wetu wazoefu Shomari Kapombe na Mohamed Hussein kwa ajili ya mchezo wetu wa marudiano dhidi Uganda na tayari wachezaji hao wapo kambini," alisema Karia
Amrouche alizungumza na wachezaji hao baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa ambao Simba walicheza dhidi ya Horoya Ac na kuibuka na ushindi wa mabao 7-0
Ilitarajiwa nyota hao kujumuishwa kikosi cha Stars baada ya maoni, mapendekezo ya wadau na zaidi baada ya Amrouche kuwashuhudia mechi dhidi ya Horoya AC
No comments:
Post a Comment