Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan amenunua tiketi nyingine 7,000 baada ya awali kununua tiketi 2,000 wakati wa hamasa iliyoongozwa na Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo akishirikiana na Maafisa Habari wa Azam FC, Simba na Yanga.
Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa pia ameongeza tiketi nyingine 2,000 huku wadau wengine wa Wizara mbalimbali wakichangia tiketi 11,000 na sasa kufikia jumla ya tiketi 20,000.
Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo kupitia kwa Katibu wake Mkuu, Saidi Yakubu amemkabidhi Rais wa TFF, Wallace Karia kwa ajili ya kufanya utaratibu wa kuzigawa tiketi hizo zilizopatikana
Tanzania na Uganda zitachuana siku ya Jumanne, March 28 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, kwenye mchezo wa kuwania kufuzu michuano Afcon 2023
No comments:
Post a Comment