Kocha mkuu wa Simba Afunguka haya kuhusu Usajili wa wachezaji wapya - EDUSPORTSTZ

Latest

Kocha mkuu wa Simba Afunguka haya kuhusu Usajili wa wachezaji wapya

 

Habari za Simba

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Olivieira ‘Robertnho’ ameanza kupembua pumba na mchele katika kikosi chake, kabla ya kuingia katika soko la usajili wa wachezaji mwishoni mwa msimu huu 2022/23.

Simba SC italazimika kufanya usajili kama itakavyokuwa kwa klabu nyingine za Ligi Kuu na madaraja mengine Tanzania Bara, kwa lengo la kuboresha kikosi kuelekea msimu ujao wa 2023/34.

Kocha Robertinho amekiri kuanza kazi maalum ya kuwafuatilia baadhi ya wachezaji wa timu zinazocheza dhidi ya Simba SC katika michuano ya ndani na ile ya Kimataifa, ili kuwapata wale watakaoingia kwenye mfumo wake na ikiwezekana awasajili mwishoni mwa msimu huu.

Kocha huyo kutoka nchini Brazil amesema lengo lake kubwa la kufanya hivyo kabla ya kufunguliwa kwa Dirisha la Usajili mwishoni mwa msimu huu, ni kutaka kuwa na orodha ya wachezaji wenye vigezo anavyovitaka, kabla ya kukutana na Uongozi wa Simba SC ambao utakuwa na jukumu la kutekeleza usajili wa klabu hiyo.

“Kwenye kila mchezo kazi yangu haishii tu kuhakikisha tunashinda, lakini tunatafuta watu bora ambao tunawaona na baada ya hapo nawafuatilia baadae, ili kufahamu viwango vyao bora vimeendelea au aliocheza kwa ubora tulipokutana naye tu,”

“Tunafuatilia wachezaji wote wa ndani na wa nje kuangalia wapi tunataka kuongeza mtu kulingana na ubora tunaouona kwa wachezaji tulionao sasa na baadaye nitakaa na viongozi mapema kufanya maamuzi.”

Aidha Robertinho ameongeza kwa kikosi chake cha msimu ujao anataka kiwe na uwiano mzuri kwa kila nafasi kuwa na wachezaji wawili wenye ubora wa juu na unaokaribiana ili kutengeneza ushindani mzuri.

“Ukiangalia sasa kila nafasi kuna wachezaji zaidi ya wawili, nadhani namna nzuri ni kuwa na uwiano mzuri wa kikosi, tunaweza kuwa na kikosi cha wachezaji ambao kila nafasi kuna watu wawili lakini kitu muhimu hapa ubora wao uwe mkubwa hata ukilingana sio mbaya na baadaye tuwaache washindanie nafasi.”

“Nitahakikisha tunakuwa na kikosi bora sana kwa kuwa mashindano tunayoshiriki na ubora wa timu pinzani yanatulazimisha kuwa na ubora huo lakini hapa lazima tukubaliane Simba SC ina jina kubwa na lazima mchezaji tutakayekuwa naye awe na hadhi ya jina la Simba nafikiri hili ni kubwa.”

“Simba inashiriki mashindano makubwa dhidi ya klabu zingine kubwa za ndani na nje ya nchi lazima mchezaji atambue kwamba anapokuja Simba awe na utayari wa kuipigania klabu hii kubwa na sio kuja kusota benchi na kushindwa kupigania nafasi.” amesema



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz